Daktari Bingwa wa Mgongo, Ubongo na mishipa ya fahamu Dr. Othman Kiloloma kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili amesema kuwa timu ya madaktari saba imewasili kutoka Muhimbili ikiwa na daktari bingwa 1 wa usingizi wakiwa na vifaa vyote muhimu ili kuungana na madaktari Bingwa wa upasuaji Bugando kwaajili ya kuweka kambi ya tiba mkoani Mwanza.
Dr. Othman Kiloloma ameongeza kuwa dhana ya kuweka kambi Mwanza imekuja ikiwa ni hatua ya kujaribu kupunguza vifo na usumbufu unaowakumba watu wenye maradhi hayo pindi wanapohitaji tiba ambapo wengi wameshindwa kupata huduma mapema kutokana na kushindwa kuzimudu gharama kwa magonjwa hayo ambayo kila kukicha idadi ya watu wenye matatizo ya Ubongo na Mishipa ya fahamu inaongezeka. Ameishukuru sana African Barrick Gold kwa kudhamini mpango huo.
Kama upasuaji utahitaji kufanyika masaa 24 tuko tayari kwa hilo, nia ni kuwahudumia wale wote watakao jiandikisha kuwa wanamatatizo na wanahitaji tiba.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa mpango huo wa tiba, Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mkolani Mh. Stanslaus Mabula amewataka wananchi wote wenye matatizo kujitokeza kwani ni nadra sana kupata tiba kama hiyo bure bila malipo, naye akisema kuwa ni mmoja kati ya waathirika wa matatizo hayo ambapo ni hivi karibuni tu! naye ametoka kufanyiwa upasuaji wa matatizo ya mgongo katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili. Pia amewashukuru sana Madaktari hao bingwa kwa kuliona tatizo na kulitafutia ufumbuzi sambamba na kuwashukuru Kampuni ya ABG waliodhamini mpango huo.
Madaktari Bingwa watakao husika na zoezi hilo la tiba itakayo tolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando.
"Mpaka sasa tumeandaa wagonjwa 33, ambao wanahitaji oparesheni, leo kuna wagonjwa 12 ambao wamepangiwa oparesheni, watoto ni wa8 na watu wazima ni wa4". Miongoni mwao kuna wagonjwa wenye matatizo makubwa wawili, mmoja anausaa kwenye ubongo, mwingine damu imeingia kichwani" alisema Dr. Gerlard ambaye ni Bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC ambao ni wenyeji)
Mmoja kati ya akinamama waliojitokeza kwa kuwaleta watoto wao kufanyiwa upasuaji wa mishipa na mgongo.
Mtoto mmoja kati ya watoto wanao subiri tiba. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwafanikishia wale wote watakaopata tiba na wale wanao subiri tiba.
Mtoto anasubiri kupatiwa tiba kwa tatizo la kichwa kujaa maji.
Mama wa mtoto mwenye tatizo la kichwa.
Mtoto mwenye tatizo la uvimbe kwenye mgongo.
Baadhi ya akinamama wakiwa na watoto wao katika wodi wakisubiri kupatiwa tiba kwa matatizo mbalimbali walionayo.


















No comments:
Post a Comment