Wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa Mabibo bia na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala mara baada ya wasanii hao na Kampuni ya bia ya Mabibo kutembelea na kukabidhi misaada katika hospitali ya Mwananyamala.
Jackline Wolper (katikati) akimsaidia mmoja wa wagonjwa waliopo kwenye hospitali ya Mwananyamala wakati wasanii wa bongo movie walipotembelea hospitali ya Mwananyamala
Sada Abasi (kushoto) akipokea misaada kutoka kwa mmoja wa wasanii wa bongo movie ambao walitembelea hospitali ya Mwanyamala ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Kampuni ya Mabibo Bia ambao ni wauzaji wa Vinywaji vya Windhoek na Climax kwa kushirikiana na Wasanii wa Bongo Movie wametembelea hospitali ya Mwananyamala ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie ambapo Kampuni ya Mabibo Bia wakiwa wadhamini wakuu wa Bongo Movie kwenye kilele cha Kuadhimisha Miaka Mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.
Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw Steve Nyerere wameweza kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala ikiwa wanadhimisha miaka mitatu ya kuzaliwa kwa Bongo Movie.
Misaada iliyotolewa leo na wasanii wa Bongo Movie kwa kushirikiana na kampuni ya Mabibo Bia ni mabeseni ya kuoshea watoto wadogo, pampers, sabuni na mafuta ya kujipaka.









No comments:
Post a Comment