Advertisemet

.

Wednesday, 26 March 2014

MRADI BAINA YA USHIRIKIANO KATI YA CHUO CHA VETA NA UJERUMANI UJULIKANAO KAMA "GERMAN DUAL SYSTEM APPRENTICESHIP" WATAMBULISHWA.


Meneja Mradi wa “German Dual System Apprenticeship”(katikati) Martin Mac Mahon akizungumzia juu ya mradi ambao German wameshirikiana na Chuo cha VETA nchini katika kuhakikisha wanaboresha suala la elimu kwa vitendo Tanzania. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru.


Meneja Mradi wa “German Dual System Apprenticeship”(katikati) Martin Mac Mahon akiongea na waandishi wa habari wakati alipowatembeza kwenye moja ya karakana ambayo inatoa masomo kwa vitendo yaliyo chini ya mradi wa ”German Dual System Apprenticeship” iliyopo katika Chuo Cha VETA kilichopo Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.


Wanafunzi wa Chuo Cha VETA wakiwa katika mafunzo kwa vitendo ambayo yapo chini ya mradi wa “German Dual System Apprenticeship” ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo na kuunganishwa na makampuni ambao wanafunzi hao hupelekwa kwaajili ya mafunzo zaidi


Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutambulisha mradi wa ushirikiano kati ya Vyuo vya Ujerumani na VETA kwa wanafunzi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

 
Don't Forget To Join US In MalikiaTz Community
×
bloggerWidget