Afisa
habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa
Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam kuhusu waombaji kazi kujiandaa vyema ili kukidhi vigezo
vya usaili, na kushoto ni Afisa Udhibiti na Ubora wa
Sekretarieti hiyo bw. Chistopher Liganga.
Ofisi ya Rais
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuandaa programu ya Elimu kwa
umma ili kuwawezesha waombaji wa kazi kuweza kutimiza vigezo vinavyohitajika
ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata kazi walizooomba.
Hayo yamesemwa na
Afisa Habari Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Bi Riziki
amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo waombaji wa ajira kuweza kuandaa
wasifu wao vyema (CV), kuandika barua za maombi kwa ufasaha, kuwajengea
uezo wa kufanya maandalizi sahihi kabla ya usaili.
Aliongeza kuwa hali
hiyo inatokana na kujitokeza kwa changamoto za wahitimu walio wengi kushindwa
kutimiza vigezo husika ili waweze kupata ajira wanazoomba.
Bi Riziki alisisitiza
na kusema kuwa katika kutekeleza mpango huo watashirikiana na Taasisi za Elimu
hapa nchini ili kuwasaidia wanafunzi wanaohitimu vyuoni ili kuwajengea uwezo
ili waweze kukidhi vigezo mara wanapoomba ajira Serikalini.
Katika kipindi cha
miaka minne Tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma
imekabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ubora wa wahitimu wanaowasilisha
maombi ya kazi Serikalini kuanzia ngazi ya Sekondari, Stashahada ya juu,
Shahada ya uzamili pamoja na shahada ya uzamivu.
Pia Bi Riziki
alibainisha kuwa katika tathmini sekretarieti kupitia maombi ya ajira
yaliyowasilishwa wamebaini mapungufu yatokanayo na ubora hafifu wa baadhi ya
wahitimu wanaoomba kazi kupitia chombo hiki.
Dhana potofu ya
wahitimu kuwa na vyeti pekee ndicho kigezo pekee cha mhitimu kupata ajira
badala ya kuwa na uelewa mpana wa kile walichoombea kazi, kutotilia maanani
sifa na masharti ya Tangazo husika, kutojiamini,kukosa uzoefu wa kazi
unaohitajika na uwezo mdogo wakutumia lugha kwa ufasaha.







No comments:
Post a Comment