Wanawake wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakisherehekea wakati wa maadhimisho ya siku
ya Wanawake kuelekea uwanja wa mwembe yanga.
Wizara ya Mambo ya Ndani wakisindikizwa na Bendi ya Polisi wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake.
Bendi ya jeshi la Kujenga
Taifa wakiwasindikiza waandamaji katika kilele cha Siku ya Wanawake Duniani
yaliyofanyika katika Viwanja Vya Mwembe Yanga, Wilayani Temeke
Magereza hawakua nyuma
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari nao wakishangilia
siku ya wanawake duniani
Wakazi wa Jiji la
Dar es salaam wakitembelea Mabanda mbalimbali yaliyopo katika uwanja huo wa Mwembe Yanga
wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani
Doroth Kaiyuzi , Kutoka Chama cha Wasioona Akisoma
Risala mbele ya Wageni Rasmi katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake
yaliyofanyika katika Uwanja wa Mwembe Yanga, Jijini
Dar Es Salaam
Jovina Vedastus ambaye ni Fundi wa Ushonaji na utengenezaji wa
Batiki akicheza muziki pamoja na wanafunzi wenye ulemavu ambapo alikonga nyoyo
za watu wengi kwa umahili wake huo katika kucheza
Wanafunzi wa Chuo cha ufundi cha watu wenye ulemavu wa jumla, wakiwa wanafuatilia kwa umakini kinacho endelea uwanjani hapo
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi
upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi wakati wa kilele cha siku ya
wanawake duniani katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko
Mwanza.


_.png)





















No comments:
Post a Comment