Hakuwa na mtaji, alikuwa anachukua mchicha kwa mali kauli kutoka kwa mkulima, anasema "Alishindwa kuendelea na biashara hiyo baada ya mgambo wa jiji (City) kumwaga biashara yake hivyo akaamua kuachana na biashara hiyo".
Alipokuwa akiishi alikuwa ni mlinzi wa nyumba yeye na mumewe, kuna mama alikuwa akimuona kila siku na juhudi zake, hivyo akaamua kumpatia shilingi laki moja (100,000/=) kama mtaji na ndio safari yake ya maisha ikaanzia hapo. "Sijui kama yeye anakumbuka ila nampenda na kumuombea sana."
"Katika maisha yangu, nilipanga nitamsomesha mtoto wa kike hivyo watoto wangu wa kiume wao hawakwenda sekondari mpaka mdogo wao wa kike alipofanikiwa kwenda sekondari"
Alifanya hivyo kutokana na maisha aliyopitia yeye. "Mume anaweza kwenda kazini bila kujua watoto wanakula nini, ila mama hawezi kutoka mpaka wanae wale hata kama ni kunywa uji", akaongeza.
"Kutokana na juhudi zangu na maisha yalivyo magumu kwangu kuna mwanamke mwenzangu aliguswa na alizipenda juhudi zangu na aliamua kunipatia eka moja na pesa kiasi, kwa kweli namshukuru sana Mungu maana wanawake tukiwa na mapenzi tunaweza"
Baada ya hapo alijiunga na vikundi vidogo vidogo vya kina mama. Mafanikio Aliyoyapata ni ameweza kusomesha watoto, amejenga nyumba, pia ni mwalimu anafundisha mambo ya ujasiriamali na ni mwenyekiti wajasiriamali kinondoni.
Kwa sasa anafanya biashara mpaka nje ya nchi na kuitangaza nchi yetu. "Mwanamke akiwezeshwa anaweza"







No comments:
Post a Comment