Mke wa Rais mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili mjini Bahi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa taasisi ya wanawake na maendeleo (WAMA) akiwapungia mkono wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria uzinduzi huo.
Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa macho wa mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyokwenda sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilaya ya Bahi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Bahi kabla ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wakati wa sherehe hiyo ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Kebwe Stephen akitoa hotuba kwa niaba ya Wizara ya afya wakati wa uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Mwenyekiti wa WAMA akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo.
Bwana Hamis Mwege ambaye ni mwakilishi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC1) akipokea tuzo kwa niaba ya shirika hilo kwa kazi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Mke wa Rais Mama Salma kikwete akicheza ngoma pamoja na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Bahi mara baada ya uzinduzi.
Mke wa Rais mama Salma akiwaaga wananchi wa Bahi mara baada ya uzinduzi huo wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

















No comments:
Post a Comment