Advertisemet

.

Thursday, 15 May 2014

MPANGO MKAKATI WA KUONGEZA KASI YA KUPUNGUZA VIFO VYA UZAZI NA VYA WATOTO WAZINDULIWA NA RAIS KIKWETE.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akionesha jedwali la alama za ufuatiliaji wa utendaji wa huduma za afya ya mzazi na mtoto wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam. Pamoja naye ni naibu Waziri wa Afya Dkt Kebwe Stephen Kebwe.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kitabu Bibi Halima Shariff, mmoja wa wadau wa afya kutoka katika kundi la marafiki wa maendeleo. pamoja na kitabu hicho pia kuna  jedwali (score-card) la  alama za ufuatiliaji wa utendaji wa huduma za afya ya mzazi na mtoto wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na wagemi wengine wakifuatilia maelezo wakati wa  uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto

No comments:

Post a Comment

 
Don't Forget To Join US In MalikiaTz Community
×
bloggerWidget